Huduma
Huduma zetu nyingine
Moja ya shughuli za msingi za kampuni yetu, SHEMWETA INVEST AB, ni kuwasilisha mada mbalimbali za kielimu, maarifa na ujuzi katika Sekta ya Michezo na vilevile umuhimu wa mazoezi ya viungo kwa ajili ya kuimarisha afya za wafanyakazi wa makampuni na taasisi mbalimbali za umma na za watu binafsi.
Pia tuna kitengo maalum, SIAB COURIER & MOVERS, kwa ajili ya usafirishaji wa vifurushi na uhamishaji wa vitu mfano vya ofisi, makazi, kampuni n.k. - ndani ya Afrika Mashariki. Tafadhali wasiliana nasi kwa maelezo zaidi.
NUKUU: "...Na baada ya hapa (kitabu hiki) kingeweza kusaidia watu wengi kutuongoza,... Mimi ninafahamu Madaktari kadhaa katika field ya Physical Education...ambao tunao hapa, lakini hawajatengeneza impact yoyote kabisa katika jamii yetu hii! Lakini kijana huyu katika kipindi kifupi ameshatunga vitabu vingi. Yeye (Shemweta) ni rasilimali kwa nchi hii."
-Mh. Iddi O. Kipingu, (aliyekuwa) Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Tarehe 24/7/2010, mjini
Dar Es Salaam - Tanzania.
NUKUU: "Tumeridhishwa sana na mchango wa Alfred (Shemweta) ambapo amekuwa akionyesha moyo wa kujituma na kila mara akiwa na mtizamo chanya na hatimaye kupelekea mafanikio. Vivyo hivyo Alfred ni msimamizi mzuri na tunatumaini kutumia maarifa yake mara nyingi zaidi."
- Mkurugenzi wa Elimu, Taasisi ya Masomo na Elimu ya Michezo (SISU Idrottsutbildarna) Stockholm-Sweden, Tarehe 5/10/2003.
NUKUU: "Tuzo hii ya heshima inatolewa kwa watu ambao kutokana na shughuli zao huchangia kuitangaza Manispaa yetu, wakifanya kazi kwa malengo thabiti na matumaini mema ya wakati ujao na vilevile wakiwa mfano bora kwa kizazi kijacho hapa Huddinge."
- Manispaa ya Huddinge (Sweden) kwa ushirikiano na Jumuiya ya Makampuni Huddinge (Tuzo ya Dhahabu Mwaka 2000-Michezo.
NUKUU: "...Zipo sura (za kitabu Miongozo Yakinifu) zinazoonyesha bayana zitaweza kutoa mchango mzuri sana kwa viongozi na walimu katika medani hii. Ni vizuri wahusika katika sekta hii wakakisoma kitabu hiki."
- Maoni: Taasisi ya Elimu Tanzania (baada ya mapitio ya kitabu), Tarehe 22/8/2011.